MAKONDA AZINDUA “PEKENYUA TUKUFUKUNYUE”
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo August 29 amezindua Mpango Mkakati wa Kutokomeza Wahamihaji haramu Mkoa wa Dar es salaam alioubatiza jina la “PEKENYUA TUKUFUKUNYUE” na kuwaagiza Watendaji wa Mitaa kurejesha Daftari la Mkazi ili Kila Mkazi kuanzia ngazi ya Mtaa afahamike anapoishi na kazi anayofanya jambo litakalosaidia pia kuondoa uhalifu.
RC Makonda amesema mpango huo ni Mwarobaini tosha wa kupambana na Wageni wanaoishi Nchini kinyume na Sheria na utahusisha Watendaji wa Kata, Mitaa na Wananchi ambao watakuwa na jukumu la kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa mgeni au mtu wanaemtilia mashaka kwenye Makazi wanayoishi.
Aidha RC Makonda amesema uwepo wa Wahamihaji Haramu Nchini ni jambo la hatari kiusalama kwakuwa baadhi yao wanafanya uhalifu wa Wizi, Ubakaji, Uporaji, wanatumia rasilimali za nchi, wanatumia fursa ambazo zilipaswa kuwanufaisha wazawa ikiwemo Afya, Elimu na Ajira, kusababisha msogamano wa watu magerezani pamoja na kuwa Chanzo cha Migogo ikiwemo ya Ardhi.
Kutokana na hilo RC Makonda ameviagiza Vyombo Vyote vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Kata na Mitaa kuhakikisha Mpango huo unafanikiwa kwa 100%.
Kwa upande wake Kamishina wa Uhamihaji Mkoa wa Dar es salaam amesema wamebaini idadi kubwa ya wahamihaji haramu wanatoka mataifa ya Burundi, DRC, Somalia na Ethiopia na wamekuwa wakipendelea kuishi Mkoa wa Dar es salaam kwakuwa umekuwa jiji lenye fursa nyingi za kibiashara.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.