Nchi za Ulaya zitaongeza juhudi za kidiplomasia kuyaokoa makubaliano ya Nyuklia ya Iran yanayotetereka. Ameyasema hayo waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani baada ya kufanya mazungumzo na Uingereza na Ufaransa.
Heiko Maas amesema nchi hizo tatu zinataka kuundeleza mwamko uliotokana na mkutano wa kilele uliopita wa kundi la G7 ambapo rais Trump alionesha ishara za kuwa tayari kuzungumza na Iran.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani walijumuika pamoja na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini katika mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa Umoja wa Ulaya mjini Helsinki.
Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Umoja wa Ulaya umesema mara kadhaa kwamba umejitolea kuyaokoa makubaliano ya Nyuklia ingawa juhudi za kuulinda uchumi wa Iran dhidi ya kudhoofishwa na vikwazo vya Marekani hadi sasa ni ndogo.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.