Breaking News

PAKA WA AJABU AZUA TAFRANI MJUMBE

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya firauni! Paka wa ajabu amezua taharuki si ya nchi hii nyumbani kwa mjumbe wa nyumba kumi. 

Ndiyo; ni kwa mjumbe wa Mtaa wa Masewe, Kata ya Ilemi mkoani Mbeya, Hance Hezron Mwajoka, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.

Tukio hilo ambalo liliwaacha watu midomo wazi lilitokea hivi karibuni ambapo paka huyo alizuka nyumbani kwa mjumbe huyo akiwa amevishwa shanga kiunoni, hirizi, vitambaa vyekundu na kubebeshwa pembe za ng’ombe mgongoni.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, mke wa mjumbe huyo, Kisa Swata alisema, Agosti 21, mwaka huu saa tano usiku alitoka nje kumwandalia mumewe maji ya kuoga ndipo alipokutana na paka huyo. Alisema; alipomuona hakuamini, ikabidi amuite mumewe naye alipofika akaona maji yamezidi unga ndipo alipoamua kuwaita majirani waje washuhudie maajabu.

“Heeh! Mhh!! Aisee, hii kali.” Miguno ya aina tofauti ya baadhi ya majirani ilisikika eneo la tukio. Kama ujuavyo tena mambo ya Uswahilini; tayari imani za kishirikina ziliingizwa; wajuzi wa mambo walisema paka huyo ‘mwenye vifaa tishio mwilini’ afunikwe na ndoo, lengo ni kumhifadhi hadi asubuhi ifike.
Mapema alfajiri watu walifungua ndoo hiyo na kumkuta paka huyo mzima wa afya ambapo alianza kuwatazama mashuhuda kwa jicho la aibu. Shuhuda Gabriel Mwakasula alijikuta akisema: “Huyu paka siyo wa kawaida, mbona ukimwangalia anaona aibu?”

Hapo sasa imani za kishirikina zilizidi kupamba moto miongoni mwa majirani waliofika nyumbani kwa mjumbe huyo ambapo mmoja wa majirani aliamua kuchukua shoka na kumkata kichwa. Ajabu nyingine kwa paka huyo ni pale watu walipotarajia kuwa damu zitatoka baada ya kukatwa kichwa lakini haikutoka hata tone moja.

“Jamani mbona hatoi damu?” Jirani mmoja alisikika akiwauliza wenzake waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa mjumbe huyo. Hata hivyo, baadhi ya vijana jasiri hawakutishwa na hali hiyo ndipo walipoamuru moto na mafuta yaletwe ili paka wa ajabu achomwe moto.
Inaelezwa kuwa, hata pale moto na mafuta yalipoletwa na paka kuchomwa moto hakuungua badala yake ilikuwa kama kapakwa masizi tu. “Duh!, Loh!, Mmm!” Miguno kwa baadhi ya majirani ilisikika tena baada ya paka kugoma kuteketea kwa moto.

Pamoja na yote; mambo mengine yanahitaji uamuzi mgumu, ndipo baadhi ya watu walishauri kuwa paka huyo ateketezwe kwa moto na tairi la gari na jambo hilo lilipofanyika hakukuwa na namna zaidi ya paka huyo kuteketea.

Baadaye wananchi hao walikwenda nyumbani kwa Diwani wa Kata ya Ilemi, Furaha Mwandalima kwa ajili ya kumweleza kilichotokea lakini hawakumkuta.

Mwandishi wetu alipomtafuta diwani huyo na kumuuliza anazungumziaje imani za kishirikina kwenye mtaa wake alisema: “Mara kadhaa nimeshaletewa kesi kama hizi za matukio ya kishirikina lakini mimi nawaasa watu wangu imani hizi tuzipuuze

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.