RAIS TRUMP AFUTA ZIARA YA KWENDA POLAND
Hatua ya rais Donald Trump wa Marekani ya kufuta ziara yake ya kwenda nchini Poland ili ashughulikie juhudi za kukabiliana na kimbunga Dorian nchini mwake, imepokelewa kama pigo kubwa kwa serikali ya siasa kali ya Poland ambayo imekuwa ikiitazama ziara hiyo kama hatua itakayoiweka katika nafasi ya juu kabla ya uchaguzi utakaofanyika Oktoba nchini humo.
Rais Trump badala yake amemtuma makamu wake Mike Pence kwenda Poland siku ya Jumapili katika maadhimisho ya kumbumbuku ya kuanza kwa Vita vya pili vya dunia.
Katika ziara hiyo Makamu wa rais Penye pia atakutana na viongozi wa Poland Jumatatu ambapo kikao hicho kinatarajiwa kugusia masuala kadhaa ikiwemo makubaliano mapya ya kijeshi na Nishati.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.