Breaking News

RC MBEYA ADAI WALIOSHAMBULIA KWA MAWE MSAFARA WA DC KYELA WAMECHAGUA KUUAWA

Mkuu wa Mkoa Mbeya, Albert Chalamila, ametoa onyo kali kwa watu walioshambulia kwa mawe msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudi Kitta, siku mbili zilizopita kwa kuwa wamechagua kuuawa.
Akihutubia wananchi katika Kata ya Ghana Jijini Mbeya, RC Chalamila amesema jeshi lake lipo tayari kukabiliana na watu hao wenye vitendo viovu kama hivyo.
RC Chalamila amesema endapo watarudia “Ni mkong’oto usiku kucha, Na nimesema kwa sababu kwa sababu walirusha mawe na walichagua kumuua Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Hawa wamechagua kuuawa wao, na hili nalisema na wala sio kinyume cha haki za binadamu“.
Na hili nawambieni ukweli na hapa bado sijakunjua kikosi kingine, Mnajua hapa Mbeya kuna vikosi vipo stand up, Huwa vimenyamaza, vinasubiri tu watu wajifanye.” amesema RC Chalamila.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Mapenzi na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Siasa na Burudani.