Breaking News

TANZIA: WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ZAMANI AFARIKI DUANIA


WAZIRI wa Mambo ya Nje wa zamani katika serikali ya awamu ya kwanza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyoongozwa na Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Ibrahim Kaduma, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Mtoto wa marehemu, Imani Kaduma amesema kuwa baba yake amefariki usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Agosti 31, 2019, nchini India ambako alikwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Kaduma alizaliwa mwaka 1937 katika Kijiji cha Mtwango wilayani Njombe mkoani Iringa (wakati huo) na kusoma katika vyuo Vikuu vya Makerere cha Uganda na Unn of York cha Uingereza.

Alikuwa mtaalam wa masuala ya uchumi na siasa na alihudumu katika kiti hicho cha Uwaziri wa Mambo ya Nje kuanzia mwaka 1975-1977, Waziri wa Biashara mwaka 1980-1981, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano 1981-1982. Makamu Mkuu  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  1977-1980.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.