ADA YAZUIA MATOKEO YA WANAFUNZI 8,500 UDOM MATOKEO YAO YAZUIWA
Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimezuia matokeo ya wanafunzi zaidi ya 8,500 wa shahada ya awali na ya juu kutokana na sababu mbalimbali.
Wanafunzi hao ni wale ambao hawajamaliza ada, kufuata utaratibu wa kusaini ada inayotoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na kusababisha fedha hizo kurejeshwa katika chombo hicho cha mikopo.
Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazary aliiambia Mwananchi chuoni hapo jana kuwa uamuzi wa kuzuia matokeo hayo ni wa kikao cha 71 cha seneti ya chuo kilichofanyika Septemba 6.
“Wanafunzi ambao matokeo yao yamezuiwa ni 8,329 wa shahada ya awali na 418 wa shahada ya juu ambao ni kutoka college zote saba za Udom,” alisema Baltazary.
“Wanafunzi wengine hawajakamilisha taratibu za chuo kama kulipa ada. Si kwamba wote hawana ada ila wengine hawajasaini ada zilizotoka bodi ya mikopo.”
Hata hivyo alisema hakuna mwanafunzi atakayefukuzwa kwa kutolipa ada, bali hawataruhusiwa kuona matokeo hadi alipe ili aweze kufanya mitihani atakayokuwa amefeli.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.