Breaking News

FAHAMU MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAEPUKA KATIKA UFUGAJI WA KUKU


Ndugu mfugaji ni ukweli usiopingika wala kujadilika kuwa katika ufugaji kuna baadhi ya mambo wafugaji tunayafanya lakini hayakupaswa kufanyika,

Yafuatayo ni ya kujiepusha nayo katika ufugaji:-
Kuacha banda chafu, Yapo magonjwa mengi ya kuku ambayo chanzo chake kikubwa ni uchafu unaotokana na kuku wenyewe, vitu kama vile chakula kilichokaa muda mrefu bila kuliwa na kuku wenyewe, kinyesi cha kuku na uchafu mwingine ukikaa bandani ,muda mrefu pasipo kutolewa huwa na madhara makubwa sana kataika ufugaji wa kuku.

Kuleta kuingiza kuku wageni bila kujua historia ya chanjo walipotoka. Unapofanya kitendo hicho basi ujue fika kwamba kuna uezekanao mkubwa wa kuleta magonjwa katika kuku wako, hivyo unashauriwa kwamba usiwachanganye kuku wako na kuku wengine wapya ili kuepusha magonjwa kwa kuku wako walikuwapo bandani.

Kuuza kuku wagonjwa, bila shaka utakuwa umekuwa ukiona wengi wanauza kuku wao kwa sababu wameugua. Lakini ukweli ni kwamba tunashauriwa na watalamu wa kilimo na ufugaji ya kwamba tusipendelee kuwauza kuku ambao ni wagonjwa kwa sababu hatujui madhara yatakayompata mlaji wa kuku mara baada ya kula nyama ya kuku ambayo chanzo chake ilikuwa ni ugonjwa.

Kuchinja kuku wagonjwa.
Kununua kuku wagonjwa.
Kutupa kuku waliokufa porini.
Kutibu kwa mazoea bila kuwasiliana na Afisa Mifugo.
Kutembelea mabanda ya jirani bila kuchukua tahadhari.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.