HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MBIONI KUANZISHA TAASISI YA MOYO
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) ipo mbioni kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kuhudumia wananchi wa kanda ya ziwa.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo Prof. Abel Makubi amesema kuwa wapo mbioni kuanzisha taasisi hiyo itakayokuwa na majengo mawili yenye ghorofa kumi na kumi na tano, kukamilika kwa majengo hayo wanatarajia kutumia Tsh. Bilioni 59.
“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kutoa huduma zote za kibingwa na bobezi hapa nchini,hii itapunguzia mzigo serikali na wizara kupeleka wagonjwa nje ya nchi vilevile wananchi wa kanda hii kunufaika na huduma za moyo huku huku”.
Kwa upande wa watumishi Prof. Makubi alisema wameweza kuongeza wataalam wa fani mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwepo wauguzi,madaktari,madaktari bingwa na bobezi na hivyo kufanya kazi ya utoaji huduma katika idara zote bila kuteleleka.
Hata hivyo ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kusomesha madaktari bingwa na bobezi kutoka hospitali hiyo na hivyo kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za kibingwa ikiwemo matatizo ya tumbo,mifupa,koo,pua na ndomo, macho ,mfumo wa mkojo,meno,ubongo na mishipa ya fahamu pamoja na matatizo ya akina mama.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.