Breaking News

KICHUYA AANZA VEMA MISRI

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Kiungo mshambuliaji Mtanzania, Shiza Ramadhan Kichuya, anayekipiga katika timu ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Misri Karina Klabu ya Pharco FC, amesema kuwa mpaka sasa amehusika katika michezo sita ambayo timu hiyo imecheza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya utakaoanza wiki ijayo.

Kichuya ambaye alijiunga na timu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka minne, ameeleza kuwa ndani ya mechi hizo sita tayari ameshaingia kambani mara mbili.

Kichuya amefunguka zaidi na kuseka kuwa licha ya kufunga mabao mawili, pia amekuwa akipata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi na Kocha wake akifurahishwa naye.

"Mimi huku naendelea vizuri kwakweli, tunajiandaa na msimu mpya hivi sasa na tayari tumeshacheza jumla ya mechi za maandalizi.

"Katika mechi hizo sita nimefanikiwa kufunga mabao mawili kwenye michezo tofauti na Mwalimu anafurahia maendeleo yangu, namshsukuru Mungu.

"Mazingira kwa huku nimeshazoea kwakweli, nishakuwa mwenyeji na nishazoeana na wachezaji wenzangu, changamoto zilikuwepo mwanzoni wakati naenda kwa mkopo ENPPI", alisema Kichuya.

Ikumbukwe kuwa Kichuya kabla hajajiunga na Pharco alipelekwa ENPPI inayoshiriki Ligi Kuu Misri na baada ya kumalizika muda wake sasa amerejea Pharco alikosajiliwa kuanza kazi.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.