Breaking News

MABADILIKO YA RATIBA MECHI YA SIMBA VS MTIBWA SUGAR


Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulipangwa kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru September 17 mwaka huu umerudishwa nyuma na sasa utapigwa Septemba 13, siku ya Ijumaa kwenye uwanja wa huo huo wa Uhuru.

Uongozi wa Simba umethibitisha kupokea taarifa za mabadiliko hayo yaliyofanywa na Bodi ya Ligi.

Baada ya mchezo huo, mchezo wa Simba utakaofuata ni dhidi ya Lipuli FC Septemba 22 nao ukipigwa uwanja huo huo wa Uhuru.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.