Breaking News

MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA LEO JUMAMOSI

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Klabu ya Kagera Sugar imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuwachapa wenyeji, Mbao FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni kiungo Awesu Awesu aliyefunga bao hilo pekee kwenye dakika ya 38, kikosi cha kocha Mecky Mexime kikishinda mechi ya tatu mfululizo na zote ugenini.

Hiyo ni baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma kabla ya kuwapiga 2-1 Alliance FC Uwanja wa Nyamagana hapo hapo Mwanza kwenye mechi zake mbilo zilizopita. 

Mechi nyingine ya Ligi Kuu, Bao la mshambuliaji mkongwe, Hussein Javu liliwanusuru wenyeji Ndanda SC kuchapwa na Singida United nyumbani Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kufuatia Frank Zakaria kuanza kuwafungia wageni dakika ya tano.

Nayo Mbeya City imetoa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Peter Mapunda akianza kuwafungia wenyeji dakika ya 18 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kabla ya George Chota kujifunga dakika ya 37 kuwapa wageni bao la kusawazisha.

Mechi nyingine mbili za Ligi Kuu leo zote zimemalizika kwa sare za bila mabao, JKT Tanzania na Mtibwa Sugar Uwanja wa Meja Isamuhyo na Namungo FC dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.