MFANYABIASHARA ATEKWA, AJERUHIWA VIBAYA KICHWANI
Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Innocent Shirima (pichani), mkazi wa Salasala jijini Dar es Salaam, ametekwa na watu wasiojulikana kisha kutupwa kwenye kichaka kilicho kando ya barabara.
Innocent ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Vunjo mwaka 2015, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushindwa kwa kura kiduchu na James Mbatia, aliliambia Uwazi kuwa, alifanyiwa unyama huo Septemba 4, mwaka huu.
TUKIO LILIVYOKUWA
Mfanyabiashara huyo mwenye maduka kadhaa jijini Dar ya bidhaa mbalimbali vikiwemo vifaa vya ujenzi alisema: “Baada ya kumaliza shughuli zangu majira ya saa nne usiku, niliwasha gari langu kwenda kwenye mgawaha uliopo karibu na moja ya sehemu yangu ya biashara.
“Si mbali na ninapoishi. Nilipomaliza kula wakati narudi nyumbani kwa mbele kidogo nilimuona kijana kama anahangaika kuwasha pikipiki yake. “Nilipokaribia alijitokeza kijana mwingine na kuwa kama ananiomba msaada; ikabidi nisimamishe gari nimsikilize.”
APIGWA NA KITU CHEPESI USONI
Innocent aliongeza kuwa kitendo cha kushusha kioo ili amsikilize kijana huyo, lilikuwa ni kosa kubwa kwake kwani alijikuta akipigwa na kitu chepesi mfano wa kitambaa usoni na kupoteza fahamu ghafla. “Nahisi kitambaa hicho kilikuwa na madawa ya kulevya, kwani baada ya kuzimia walinichukua na gari yangu na kunipeleka kusikojulika.
AZINDUKIA KICHAKANI
Innocent anaendelea kuliambia Uwazi kuwa matukio yaliyoendelea nyuma baada ya yeye kupoteza fahamu hayakumbuki; zaidi ya kuzinduka na kujikuta yuko kichakani eneo la Njia Panda ya Kawe, Ukwamani na Kawe Beach karibu na Hoteli ya Pikolo.
Mfanyabiashara huyo anaeleza kuwa, baada ya kutelekezwa katika mazingira tatanishi na watekaji wake kutoweka walipita vijana wawili wakiwa kwenye pikipiki ambao baadaye walimsaidia.
SIMULIZI YA WALIOMUOKOTA
Innocent anaeleza kuwa, baada ya kupata fahamu na kujikuta akiwa na majeraha ya kutisha kichwani na mwilini yanayosadikiwa kutokana na kukatwa mapanga na watekaji ndipo vijana waliomuokota walipoanza kumpa simulizi ya kusikitisha.
“Sikuwa katika ufahamu timamu lakini wale vijana wanasema mara ya kwanza walipopita kwenye barabara walikuta gari yangu ikiwa kando imefunguliwa milango yote minne, wakajua kutakuwa na tukio.
“Ikabidi wapite bila kusimama, waliporudi wakakuta hali iko hivyo, wakashauriana waje karibu ndiyo wakanikuta nimezimia huku nikiwa na majereha makubwa yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.
“Mwanzo wale vijana walipanga waniache kwa kuhofia wakitoa taarifa watakamatwa wao, lakini Mungu mkubwa wakajipa moyo na kusema liwalo na lilwe ndiyo wakaanza kuita wapita njia wengine ambapo walifika na kuanza kunifunga majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.”
APATA UFAHAMU KAMILI
“Huduma waliyonipa iliniwezesha kurejewa na fahamu ambapo niliona damu nyingi zikiwa zimetapakaa mahali hapo, jambo lililonifanya niamini kuwa nilikuwa nimecharangwa mapanga.
“Nikakumbuka wale vijana walivyoniteka wakati nikielekea nyumbani, basi niliwashukuru wale vijana walionikoa na kuwaambia kuwa ninaweza kuendesha gari kwenda Kituo cha Polisi Kawe kutoa taarifa; wale vijana walikubali kuongozana nami kama sehemu ya kuendelea kunipa msaada.”
