Breaking News

MKUU WA JKT APELEKWA MGAMBO, MBUGE AULA

Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kumteua bosi mpya wa jeshi hilo na kumhamisha aliyekuwepo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam amesema Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT.

Jenerali  Mabeyo amesema aliyekuwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la akiba (mgambo).

Busungu aliyeteuliwa kushika wadhifa wa juu ndani ya JKT, Februari 16 mwaka 2018 alichukua nafasi ya Meja Jenerali Michael Isamuhyo ambaye   alistaafu.

Aprili 13, 2019 wakati Rais Magufuli akizinduzi  mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma,  alitangaza kumpandisha cheo Mbuge kutoka Kanali na kuwa Brigedia Jenerali kutokana na kazi nzuri  aliyoionyesha ya kusimamia ujenzi huo.

Mara baada ya kumtangaza, alimuita mbele Brigedia Mbuge kwenda kukaa kwenye jukwaa kuu sehemu inayotengwa kwa ajili ya viongozi wakuu na siku hiyo hiyo eneo hilo, Mbunge alivalishwa vyeo vya Brigedia Jenerali.

Chanzo: Mwananchi.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.