Breaking News

PICHA: MASHABIKI BUKOBA WAKWAMA KUSHUHUDIA MAZOEZI YA SIMBA

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Kikosi cha Simba kimewasili mapema leo mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Alhamisi ya September 26-2019.

Jioni Simba imetumia uwanja wa Kaitaba kufanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao utapigwa hapo Kaitaba.

Licha ya mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia mazoezi hayo, hawakuweza kwani uongozi wa Simba haukuruhusu mashabiki kuingia uwanjani ili kuepuka hujuma.

Kagera Sugar imekuwa ikitoa upinzani kwa Simba misimu ya karibuni, hali hiyo imepelekea mabingwa hao wa Tanzania Bara kuuchukulia mchezo huo kwa umakini.

Aidha uongozi wa mkoa wa Kagera umeipa maadalizi maalum timu ya Kagera Sugar ili kuhakikisha inapata ushindi hapo kesho.

Inaelezwa kuwa hapo kesho timu hiyo itasindikizwa hadi uwanjani na msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Manispaa.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.