Breaking News

TUNDU LISSU AWATAJA WATAKAOMSINDIKIZA KURUDI TANZANIA

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amesema taasisi na watu mbalimbali wamejitokeza kutaka kumsindikiza, pindi atakapotaka kurudi Tanzania, itakapofika mwezi wa 10.

Tundu Lissu ameeleza hayo kupitia andiko lake akieleza miaka 2 ya tangu aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma, na kusema kipindi cha miaka 2 kilikuwa cha kipindi cha mateso na matumaini.

"Kuna wawakilishi wa taasisi za Kidini na Kijamii, ndani na nje ya nchi yetu Wanadiplomasia kutoka nchi rafiki na Mashirika ya Kimataifa, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari vya Kimataifa, ambao wameonesha nia ya kunisindikiza katika safari yangu ya kurudi nyumbani." ameandika Tundu Lissu.

"Katika mazingira haya, kurudi kwangu nyumbani hakuwezi kufanywa siri ni muhimu, kwa hiyo, tarehe ya kurudi kwangu nyumbani ijulikane wazi kwa kila mtu." ameandika Tundu Lissu.

Awali Lissu alitangaza kurudi nchini Septemba 7, 2019, lakini imeshindikana kwa kile alichokidai kuwa Daktari wake amemtaka kukutana naye mwezi wa 10.

Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.