VIDEO: HISTORIA YA KARUME, RAIS ALIYEZAWADIWA KIFO KWA WEMA WAKE!
Mwaka alfu mia kenda na tano, alizaliwa Abeid Amani Karume katika ardhi ya Zanzibar kuwakomboa wanyonge kutoka kwenye mikono katili ya Sultan aliyewatumikisha kwa jasho na damu tangu enzi na enzi, kwa jina la Karume wanyonge wakavua unyonge wao na kukavaa Uzanzibar, wakatibiwa pamoja, wakasoma pamoja, wakaishi pamoja, wakaabudu pamoja, wakaoana pamoja, wakajenga uchumi wao pamoja, Zanzibar maisha yakapata maana.
Hata hivyo kilichomuondoa Sultan katika hivyo visiwa vya marashi ya karafuu si uraia wake bali ni dhuluma aliyowafanyia waswahili tangu utawala wa kisultani uingie Zanzibar. Ilikuwa 1698.
Katika utawala huo mweusi aliwekwa katika daraja moja na mbuzi, samaki, nazi, karafuu na ardhi ndo maana aliuzwa utumwani na kumilikiwa kama bidhaa.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.