YANGA YAMKATIA RUFAA ZAHERA
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umemkatia rufaa kocha wake Mwinyi Zahera kupinga kufungiwa kutokana na madai ya kutoa lugha chafu kwa Bodi ya Ligi.
Bodi ya Ligi ilimfungia Zahera kutoitumikia timu yake kwa mechi tatu na kupigwa faini ya laki tano (500,000) kutokana na kutovaa nadhifu.
Akizungumza na Gazeti la Championi Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema jana kuwa, tayari wameshaka rufaa na wamepeleka barua ndani ya Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili waweze kutoa maamuzi sahihi.
“Maamuzi mbalimbali ya TFF na Bodi ya Ligi hayapo sahihi, kuna mambo mawili ambayo yamejitokeza ya kumfungia kocha wetu kutocheza mechi tatu na penalti aliyoipata ya kutakiwa kulipa Sh 500,000 kutokana na madai ya kutovaa kwa unadhifu.
“Ukiangalia kanuni suala nadhifu linaangalia usafi, uvae nguo ambayo ni safi. Hivyo suala la kuvaa pensi ni la kawaida kwani tumeweza kushuhudia wachezaji, waamuzi, na hata duniani kwote pensi ni vazi la kawaida hivyo tumeangalia kwa ujumla wake na tumeona kama klabu tumekosea wapi.
“Tumelikatia rufaa tuone tumekosea wapi tumepeleka malalamiko yetu kwenye Bodi ya Ligi na TFF kwa kuwapatia barua ili waweze kupitia nakutoa maamuzi sahihi na kutoa tafsiri ya unadhifu.
“Kocha wetu alizungumza maneno sahihi na sisi kama uongozi tunamuunga mkono ni maneno sahihi kwa kudai kuwa timu yetu ilishindwa mchezo uliopita kunatokana na wachezaji kuchoka, tuliwaandikia barua TFF, Bodi ya Ligi na kwa waziri ili mechi isogezwe lakini walitukatalia.
“Tunaomba TFF wamwite mwalimu aweze kupata haki ya kusikilizwa kwa mujibu wa kanuni za TFF na sheria za nchi, unapotaka kutoa hukumu lazima mwalimu asikilizwe na kama kuna uongo ambao mwalimu ameuzungumza basi uongozi tutakuwa tayari kukubaliana na TFF,” alisema Mwakalebela.
Aidha Mwakalebela ametangaza viingilio vya mechi dhdi ya Zesco wanayotarajia kukutana nao Septemba 14, kuwa mzunguko itakuwaSh 5,000, Sh 30,000 kwa VIP A na 100,000 kwa VIP B.
Usikubali kupitwa na chochote kile tembelea App hii kila mara kupata Habari zote zinazojiri Tanzania na nje ya Tanzania katika Michezo, Magazeti, Mahusiano, Elimu, Ajira, Video, Audios, Tamthilia na Udaku.