Breaking News

AS ROMA KUANZA KUTUMIA KISWAHILI

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Klabu ya soka ya AS Roma ya Italia, Huenda ikawa klabu ya kwanza kutoka katika ligi kubwa 5 barani kuanza kutumia lugha ya kiswahili kwenye kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, Kwani imetangaza kuanza zoezi hilo mapema iwezekanavyo.
Klabu ya Roma jana iliandika ujumbe wa kumpongeza mwanariadha kutoka Kenya, Eliud Kipchoge ambaye aliweka historia ya kuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za nyika kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya masaa mawili.
AS Roma waliandika “INCREDIBBLE” na ndipo watu wengi hususani kutoka Kenya walianza kumlazimisha Admin wa Akaunti hiyo ya Twitter, Ku-tweet kwa lugha ya kiswahili na wengine wakiomba klabu hiyo ifungue akaunti rasmi ya Kiswahili.
Baada ya malalamiko hayo, AS Roma walijibu kwa kiswahili kwa kuandika “Admin amefurahi, asante wote, mnanifundisha swahili Lala salama”.
Kufuatia maombi hayo, Tayari Rais wa Klabu hiyo, Bilionea James Joseph Pallotta amesema kuwa maombi hayo yamepokelewa na muda si mrefu watafungua ukurasa wa Kiswahili.
Kama mnahitaji ukurasa wa As Roma wa Kiswahili kweli mnastahili kuwa nao. Unawajia muda si mrefu. Amani na upendo kwenu nyote.” ameandika Pallotta kwa Kiswahili kwenye ukurasa wake wa  Twitter.

Kama mnahitaji ukurasa wa As Roma wa Kiswahili kweli mnastahili kuwa nao.

Unawajia muda si mrefu.

Amani na upendo kwenu nyote.
615 people are talking about this
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.