FARAJA NYALANDU ALAMBA SHAVU
Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Miss Tanzania 2004, Faraja Nyalandu na mwanamuziki Grace Matata wamelamba shavu la ubalozi wa Kampuni ya Usafiri wa Anga ya Travelstart katika kampeni ya kuwafikia wateja kwenye huduma zitolewazo na kampuni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Meneja wa Travelstart, Robert Othman alisema wameamua kufanya kampeni hiyo ili kuweza kupanua huduma kwa wateja kwa kuwafikia kwa haraka popote walipo watumiapo mitandao.
“Tumeamua kufanya kampeni hii kwa muda wa miezi miwili, kutakuwa na mashindano kwa watu wote, hii tumeona ni njia pekee ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuwa nasi kwa kipindi kirefu. Kwenye matangazo yetu ya barabarani, endapo mtu akipita maeneo yenye matangazo yetu, akiona mdudu aina ya nyuki, kipepeo na konokono apige picha na atume kwenye mtandao wetu atakuwa amejipatia fursa ya kusafiri kwa gharama za kampuni yetu.
“Safari hizo kwa washindi watasafiri kwa muda wa siku mbili, kwa wale ambao watapata bahati ya kwenda nje ya nchi na nchi ambazo watakwenda ni Thailand, Jordan, Amsterdam, Dubai au Mauritius na kwa mikoa ya hapa tutaangalia huenda tukasafirisha kwenda labda Ngorongoro, Serengeti, Zanzibar na sehemu nyingine,” alisema meneja huyo.