LISSU ASISITIZA KUGOMBEA URAIS
Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.
ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA
HAKIKISHA UMEUPDATE
MWANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesisitiza nia yake ya kugombea urais, iwapo atapata wito kutoka kwa wananchi na chama chake kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza na VoA nchini Marekani, alisema: “Nimeshatangaza utayari wangu wa kugombea nafasi hiyo nikiteuliwa na chama changu na ninarudia tena nikipata wito wa kugombea urais nitapokea wito huo.”
Lissu ambaye yupo nje ya nchi tangu Septemba 7, mwaka juzi kwa ajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi, alisema hayo licha ya hivi karibuni kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini akieleza kuwa hatarejea nchini hadi hapo chama chake kitakapomhakikishia usalama wake.
Akieleza kuhusu malengo yake iwapo atafanikiwa kuteuliwa na chama chake kugombea urais, Lissu alisema atarejea upya mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya wananchi ili kuwapatia wananchi katiba bora.
Kauli hiyo ya Lissu kuhusu kugombea nafasi ya urais amekuwa akiirudia mara kwa mara, licha ya kuugua kwake na hivi karibuni kudai kuwa hatarejea nchini.
Kauli hiyo ya Lissu kuhusu kugombea nafasi ya urais amekuwa akiirudia mara kwa mara, licha ya kuugua kwake na hivi karibuni kudai kuwa hatarejea nchini.
Lissu ambaye amekuwa mbunge kwa vipindi viwili, alivuliwa ubunge wake kutokana na sababu iliyotolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai za utoro bungeni na pia kutojaza fomu za maadili ya watumishi wa umma, ambazo hutakiwa kujazwa pia na wabunge wote.
Lissu alifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kudai ubunge wake kwa kile alichodai Spika kukiuka taratibu za uamuzi wa kumvua ubunge, hata hivyo, alishindwa katika kesi hiyo.