Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA HAKIKISHA UMEUPDATE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amedai kuwa vitalu vingi vya uwindaji wa wanyamapori nchini vimekosa wawekezaji na hata baadhi ya wawekezaji waliokuwa wanamiliki baadhi ya vitalu hivyo kulazimika kuvirudisha Serikalini kwa kukosa wanyamapori.
Mhe. Constantine Kanyasu
Kanyasu amesema kuwa sababu kubwa iliyopelekea tatizo hilo ni mifugo kuingizwa ndani ya hifadhi na kuwafanya wanyamapori wengi kuhama.
Akizungumza katika Pori la Akiba la Moyowosi-Kigosi na watumishi wa kituo cha Ipole Kaskazini mwa pori hilo kwa upande wa Geita, Waziri Kanyasu amewataka watumishi hao kuimarisha ulinzi kwa kufanya doria madhubuti, ili kuzuia wafugaji wasiweze kuingiza ng’ombe katika pori hilo.
Naibu Waziri amesema Wanyamapori hulazimika kuhama maeneo yaliyovamiwa na Ng’ombe na Mbuzi kwa sababu hushindwa kuvumilia harufu madawa ambayo hutumika kuoshea wanyama hao.
Kufuatia hali hiyo, Vitalu vingi vimekuwa havina wanyamapori na badala yake, vimekuwa na ng’ombe hali inayosababisha wawakezaji wengi kuvirudisha vitalu hivyo kwa kukosa wanayamapori.
Kanyasu amesema mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu, Jumla ya vitalu 60 kutoka mapori ya akiba mbalimbali vilikuwa vimerudishwa serikalini kutoka kwa wawekezaji.
Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.
NG’OMBE, MBUZI KIKWAZO CHA WAWEKEZAJI WA VITALU
Reviewed by
on
October 13, 2019
Rating: 5