Breaking News

PSG YATHIBITISHA KUMKOSA NEYMAR KWA MUDA HUU

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Paris Saint-Germain, Neymar atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne kufuatia kupata majeraha katika mchezo wa kirafiki baina ya timu yake ya taifa ya Brazil dhidi ya Nigeria.
Image result for Neymar out of injury for four weeks
Paris Saint- Germain, imetoa taarifa hiyo hapo jana siku ya Jumatatu kwa kukosekana kwake kwa muda huo wa wiki nne kutokana na kupata majeraha hayo nakutolewa ndani ya dakika ya 12 ya mchezo wakati walipotoka sare ya mabao 1 – 1 dhidi ya Nigeria siku ya Jumapili.
Kama atakuwa nje mpaka Novemba 11, Neymar atakuwa ameikosa michezo minne ya ligi kuu Ufaransa ikiwa ni pamoja na safari ya kuwafuata Marseille Oktoba 27 ikiwa ni pamoja na mechi ya nyumbani na ugenini ya Champions League dhidi ya Bruges.
Kama ratiba ya matibabu yake itakwenda kama ilivyokusudiwa basi nyota huyo atarejea uwanjani kwenye mchezo  dhidi ya Real Madrid na hivyo wanapaswa kujipanga vizuri kumkabili mchezaji huyo, pale katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu, Novemba 26.
Mchezaji huyo ghali zaidi duniani amekuwa akikutana na majeraha mara kwa mara hivyo kushindwa kuonyesha uwezo wake kwa muda mrefu zaidi na hata kutotoa mchango wa kutosha kwa matajiri hao wa Ufaransa hasa ukilinganisha na uwezo wake.
Image result for Neymar out of injury for four weeks
Kwa mwaka huu pekee Neymar amepata majeraha zaidi ya mara moja, mwezi Januari alishidiwa pia nyota huyo akikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.