Breaking News

SIMBA YAENDELEA UBABE LIGI KUU, AZAM YAAMBULIA KICHAPO

Klabu ya Simba SC imeendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya kubuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo katika dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Miraj Athumani ‘Madenge’ au Sheva dakika ya 39 akimalizia pasi ya kiungo mahiri Muzamiru Yassin.

Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems inafikisha pointi 18 katika mchezo wa sita ikiendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 💯.

Hali ni mbaya kwa Singida United ambayo leo imepoteza mechi ya tano kati ya nane, nyingine tatu zote ikitoa droo, hivyo kuendelea kushika mkia. 


Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC bao pekee la Moses Shaaban dakika ya 68 akimalizia pasi ya Abdurahman Mussa dakika ya 27.

Nayo Biashara United ikaichapa 1-0 Namungo FC, bao pekee la Juma Mpakala dakika ya 72 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

Coastal Union wakaibuka na ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC Uwanja wa Samora, Iringa bao pekee la Andrew Simchimba dakika ya 27.

Mwadui FC ikaongoza kwa 2-0 hadi dakika ya mwisho kwa mabao ya Gerrald Mdamu dakika ya 21 na Hassan Kapalata dakika ya 39, kabla ya JKT kutumia dakika za majeruhi kupata sare ya 2-2 kwa mabao ya Edward Songo dakika ya 90+1 na Najim Magulu dakika ya 90+3.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE