Breaking News

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA UKANDA WA PWANI

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa siku mbili.

Angalizo hilo limetolewa leo Oktoba 16 na kutaja maeneo yatakayokumbwa na mvua hiyo kuwa ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa kutoka TMA zimesema mvua hizo zitaanza Oktoba 16 hadi Oktoba 17,2019 hivyo wakazi wa mikoa tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.

Kwa sababu hiyo athari zitakazotokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.