Breaking News

VIDEO: MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019 YATANGAZWA, MARA YANG’ARA KISHULE “909 WAFUTIWA MATOKEO

Baada ya kufanya maboresho katika App yetu sasa tunakuomba ufanye ku update ili kuendelea kupata habari zetu zote pamoja na kutazama mechi live, kusikiliza radio zote za Tanzania na mengine mengi katika ubora zaidi

ILI KU UPDATE BOFYA👉👉👉 HAPA 
HAKIKISHA UMEUPDATE

Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA) limetangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2019 na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78.

Image result for dkt msonde
Katibu Mtendaji wa Necta, Dkt. Charles Msonde

Akisoma matokeo hayo leo Oktoba 15, 2019, Katibu Mtendaji wa Necta, Dkt. Charles Msonde amesema tayari wameshazitaarifu mamlaka za ajira na sheria ili ziwachukulie hatua waliohusika na udanganyifu huo.
Dkt. Msonde amesema kuwa katika matokeo hayo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu, matokeo ya jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asilikia 3.78.
“Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili,” amesema Dk Msonde.
Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.
Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.
Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.
Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.
Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha.
BOFYA —>HAPA<—- KUTAZAMA MATOKEO HAYO.



Zaidi Na Zaidi Tembelea App Hii Kila Mara , Kila Saa Kupata Habari Zote Zinazojiri Tanzania Na Nje Ya Tanzania Katika Mapenzi Na Mahusiano, Elimu, Ajira, Michezo, Maisha, Magazeti, Videos, Audios, Tamthilia Na Burudani.