Breaking News

YANGA YAANZA VIBAYA KUWANIA KUZUFU MAKUNDI

Klabu ya Yanga SC imejiweka kwenye mazingira magumu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania nafasi hiyo jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Yanga sasa wanaendeleza rekodi yao ya kutoshinda mechi za nyumbani za michuano ya Afrika kuanzia Ligi ya Mabingwa ambako ushindi wa ugenini wa 1-0 uliwavusha raundi ya pili baada ye sare ya 1-1 nyumbani na Township Rollers kabla ya kwenda kutolewa na Zesco United kufuatia kufungwa 2-1 Ndola ikitoka kutoka sare ya 1-1 Dar es Salaam.

Na pamoja na kuuhamishia Mwanza mchezo wake wa kwanza mchujo wa kuwania hatua ya makundi, Yanga SC leo imeshindwa kugeuza matokeo, zaidi yamekuwa mabaya kabisa baada ya kufungwa kutoka sare za Dar es Salaam. 

Sasa Yanga SC watatakiwa kwenda kujaribu kushinda ugenini kwenye mchezo wa marudiano Novemba 3, mwaka huu Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo kwa mechi zao za nyumbani.

Katika mchezo wa leo, mabao ya Pyramids FC yalifungwa na kiungo Mburkinabe, Eric Traore dakika ya 42 na beki Omar Gaber dakika ya 63  wote
walimalizia krosi za mshambuliaji Mohamed Farouk, wakati bao pekee la Yanga lilifungwa na kiungo wake, Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Yanga SC inayofundishwa na kocha Mkongo, Mwinyi Zahera, ilimaliza pungufu baada ya beki wake mzoefu, Kelvin Yondan kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 90 na ushei.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE