ACHANA NA KIPIGO DHIDI YA KMC, PIGO KUBWA LAIKUMBA SIMBA
Achana na habari za kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC jana katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Azam Complex, uaambiwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba SC wameingiwa na hofu juu ya kuumia kwa beki Erasto Nyoni.
Nyoni ambaye amekuwa bora kwa muda wote tangu asajiliwe Simba aliumia juzi wakati akiitumikia timu ya taifa 'Taifa Stars' katika mechi dhidi ya Equatorial Guinea ambayo ilichapwa mabao 2-1 jijini Dar es Salaam.
Nyoni aliumia goti katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ni ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kuumia kwa Nyoni kunaleta hofu kwa mashabiki na wanachama wa Simba kutokana na ubora wake ndani ya dimba.
Taarifa za ndani zinasema Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ni kama ameingia na hofu pia juu ya kuumia kwa Nyoni ambaye amekuwa akianza katika mechi nyingi.
Nyoni hajajumuishwa katika kikosi cha Stars ambacho kimesafiri jana kuelekea Libya kwa ajili ya mchezo mwingine wa kuwania fainali hizo utakaopigwa Novemba 19.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE