HIZI HAPA TIMU ZILIZOFUZU 16 BORA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RAUNDI ya tano ya michuano ya UEFA Championi Ligi hatua ya makundi imeendelea tena usiku wa kuamkia November 27, 2019 kwa michezo kadhaa kuchezwa huku timu nne zikifanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Tottenham Hotspur chini ya Kocha wake mpya Mreno Jose Mourihno inafuzu kwa kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili nyuma ya FC Bayern Munich anayeongoza Kundi kwa kuwa pointi 15.
Hapo jana usiku Spurs ya Mourinho ilifanya maajabu baada ya kusawazisha na kutoka kufungwa goli 2-0 na kupata ushindi wa 4-2 dhidi ya Olympiacos.
Real Madrid na PSG nazo zimefunzu baada ya kutoka sare ya 2-2 , Real Madrid wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 8 huku PSG akiongoza kundi kwa pointi 13.
Ushindi wa 1-0 wa Juventus dhidi ya Atletico Madrid umeipeleka Juventus hatua inayofuata na licha ya Atletico kuwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 7 italazimika kusubiri hadi mchezo wake wa mwisho ili kujua hatma yake kwani FC Bayer Leverkusen iliyopo nafasi ya 3 ina pointi 6 hivyo bado ina nafasi ya kufuzu.
Sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Shakhtar Donetsk imemvusha Manchester City na Shakhtar kubaki na sintofahamu kwa kutakiwa kusubiri hadi mchezo wa mwisho ndio wajue hatma yao.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE