Breaking News

HUYU HAPA MRITHI WA AUSSEMS SIMBA


IMEELEZWA kuwa Seleman Matola kocha wa Polisi Tanzania ataibukia Simba kuchukua mikoba ya ya benchi la ufundi ambalo limevunjwa na uongozi wa Simba.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alithibitisha kuachishwa kazi jana kwa kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba ameambiwa na uongozi wa Simba kwamba yeye sio kocha tena wa Simba na baadaye uongozi wa Simba ukathibitisha kuachana naye jumla.

Habari zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Simba umefanya mawasiliano na uongozi wa Polisi Tanzania ili kupata huduma ya Matola ambaye aliwahi kuwa kocha wa Simba.

Patrick Rweyemamu, meneja wa Simba amesema kuwa ni ngumu kuzungumzia suala hilo kwa kuwalipo juu ya uongozi ila taarifa zitatoka muda wowote kuanzia leo.

Aussems aliweza kuiongoza Simba msimu uliopita kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na msimu huu alianza kubeba ngao ya jamii.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE