ISHU YA KUONDOKA SIMBA, AUSSEMS AWEKA MAMBO WAZI
Kocha Mkuu wa Klabu y Simba Patrick Aussems amesema hana tatizo iwapo uongozi wa klabu hiyo utaamua kusitisha mkataba wake lakini mpaka sasa yeye anaendelea na majukumu yake kama kocha wa Simba.
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu Mbelgiji huyo ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting ulikuwa wa mwisho kwake.
Akizungumza baada ya mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, Aussems alisema taarifa nyingi zilizoripotiwa kuhusu yeye hazina ukweli wowote.
Aidha Aussems amesema taarifa hizo pia zimekuwa zikiwachanganya wachezaji wake.
"Nyie waandishi mmekuwa mkiandika mambo mengi ambayo hayana ukweli. Wakati mwingine mmewachanganya hata wachezaji wangu"
"Nimekuwa nikipokea ofa kutoka vilabu mbalimbali kila baada ya wiki mbili lakini mpaka leo bado niko Simba"
"Nina mkataba hapa, naheshimu makubaliano yangu na klabu ya Simba. Lakini kama viongozi wa Simba wataamua kuvunja mkataba basi mimi sina tatizo," alisema Aussems
Jana baada ya mchezo mashabiki wa Simba walionyesha kumuunga mkono Aussems wakimshangilia mara baada ya mchezo kumalizika.
Baadhi ya mashabiki waliusihi uongozi wa Simba usimuondoe kocha huyo kwani bado mchango wake unahitajika kwenye klabu ya Simba.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE