JAFO ATAJA MIKOA 3 AMBAYO HAITAFANYA UCHAGUZI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, amesema kuwa takribani mikoa mitatu haitoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika kesho Novemba 24, 2019, baada ya wagombea wake kupita bila kupingwa.
"Leo ndio siku ya mwisho ya kampeni, niwaombe wananchi kujitokeza na kupiga kura lengo ni kushiriki vyema na kuwachagua viongozi kwa mstakabari wa maendeleo yao, uchaguzi huu utaendelea nchini kote isipokuwa kwenye mikoa mitatu ambayo vyama mbalimbali wagombea wake wamepita bila kupingwa ambayo ni Tanga, Katavi na Ruvuma" amesema Waziri Jafo.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE
