Breaking News

KAPOMBE AJIENGUA STARS



Beki wa Klabu ya Simba SC Shomari Kapombe ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa, #TaifaStars’,

Kapombe amesema kuwa “Kutokana na kutetereka kwa afya yangu kufuatia majeraha ya mara kwa mara, nimeona sasa ni wakati muafaka wa kustaafu kuchezea Taifa Stars na kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kuitumikia timu yetu”

Kapombe amesema yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo wakati wowote afya yake itakapoimarika.


“Pamoja na hayo nipo tayari kurejea kuitumikia Taifa Stars kama kijana mzalendo wa taifa hili tukufu pale nitakapoona afya yangu imeimarika na kwamba mchango wangu katika kikosi hicho utakuwa wenye mafanikio chanya,” imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na mchezaji huyo kwa umma.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE