MAPOKEZI YA ALIKIBA TABORA NI HATARI TU
Mapokezi ya msanii Alikiba mkoani Tabora kwa ajili ya Tamasha lake la Alikiba Unforgetable katika mkoa Tabora ni hatari tupu, haijawahi kutokea baad aya watu kufurika barabarani kwa ajili ya kumlaki msanii huyo mkubwa kutoka nchini Tanzania.

Ikumbukwe mara ya kwanza Alikiba alitangaza Tamasha hili kwenda kufanyika katika mkoa wa Mwanza ambako alitakiwa akalizindue lakini haikuwa hivyo kwani alikuja kutangaza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake Tamasha hili halitaenda kuzinduliwa Mwanza badala yake liatenda kuzinduliwa mkoani Tabora alimaarufu TORONTO.
Leo Alikiba aliondoka jijini Dar Es Salaam kuelekea Tabora na mapokezi yake yamekuwa makubwa sana.