Breaking News

MATOKEO YA SIMBA VS RUVU SHOOTING

MIRAJI Athuman leo ameendeleza pale alipoishia kwa kufunga mabao mawili ya nguvu wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shoting uwanja wa Uhuru.

Miraj alifungua akaunti ya bao lake la kwanza dakika ya 39 akimalizia pasi ya beki  wa kulia Shomari  Kapombel bao lililodumu hadi muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili Simba iliandika bao la pili kupitia kwa mbrazil Tairone Santos aliyemalizia kona ya Francis Kahata dakika ya 47 kabla ya Sheva au kupachika bao la tatu na la ushindi akimalizia pasi ya Kahata katika dakika ya 75.

Ruvu Shooting ilipambana kutafuta bao la kufutia machozi na ilifanya jaribio matata kupitia kwa Abdlhaman Mussa dakika ya 80 na haikuzaa matunda.
Ushindi huu unakuwa ni wa saba mfululizo kwa Simba mbele ya Ruvu Shooting kwenye Ligi Kuu huku Ruvu ikifunga jumla ya bao moja pekee na Simba ikifikisha jumla ya mabao 23.

Simba inabaki kilelelni ikiwa na pointi zake 25 na inaishusha Kagera Sugar nafasi ya kwanza kwa sasa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE