NYOTA YANGA KUIKOSA ALLIANCE FC
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Alliance Schools FC utakaopigwa jijini Mwanza Ijumaa ya wiki hii, mchezaji Mapinduzi Balama atakuwa nje ya dimba.
Balama atakuwa nje ya mchezo huo kufuatia kuumia nyonga katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya JKT Tanzania.
Taarifa zimesema kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amethibitisha kwamba Balama atakuwa nje ya kikosi sababu ya majeraha hayo.
Leo alfajiri kikosi cha Yanga kimeanza safari ya kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ya aina yake kufuatia Alliance kuchapwa kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Azam FC jana.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE