RC KAGERA AWASHUKIA WENYE VITI WA SERIKALI ZA MITAA
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Elisha Gaguti ametoa onyo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji katika mkoa huo watakaojihusisha na vitendo vya kuanzisha migogoro kwa lengo la kujinufaisha.
Amesema wakati mwingine viongozi hao huchochea hali ya uvunjifu wa amani ndani ya jamii jambo ambalo huchangia kuduma za maendeleo ya wananchi na mkoa kwa ujumla kudorora.
Brigedia Jenerali Gaguti ametoa onyo hilo wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha wenyekiti wa serikali mitaa 66 iliyoko katika manispaa ya Bukoba pamoja na wajumbe iliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Ihungo.
Amesema viongozi watakaoanzisha migogoro ndani ya jamii kamwe hawatavumiliwa hivyo watashughulikiwa kulingana na sheria zilizipo na baadhi ya viongozi waliozungumza wameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na mkuu huyo wa mkoa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba Maurice Limbe amewahimiza viongozi hao wasijihusishe na vitendo vya kuuza maeneo ya ardhi hasa kwenye maeneo yaliyoko kwenye ukanda wa kijani.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE