Breaking News

TANZANIA YAIFUATA KENYA FAINALI

TANZANA Bara itakutana na Kenya katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Wanawake Kesho Jumatatu November 25 Saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Hiyo ni baada ya timu hizo kushinda mechi zao za Nusu Fainali ya michuano hiyo jana, Kilimanjaro Queens wakiilaza Uganda kwa bao 1-0, huku Kenya wakiichapa Burundi 5-0 hapo hapo Azam Complex.

Bao pekee la Kilimanjaro Queens, mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano hiyo lilifungwa na mshambuliaji wake nyota, Asha Rashid Saada ‘Mwalala’ katika ya dakika ya 90 na ushei akimalizia krosi ya Mwanahamisi Omary Shaluwa ‘Gaucho’.
Kilimanjaro Queens itamenyana na Kenya katika fainali CECAFA Challenge Wanawake Jumatatu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi 
Asha Rashid ‘Mwalala’ ameifungia bao pekee Kilimanjaro Queens leo ikiilaza Uganda 1-0

Na mabao ya Kenya dhidi ya Burundi iliyochapwa pia 5-0 na Tanzania Bara katika mechi ya Kundi A yamefungwa na Dorcus Nixon dakika ya 14, Jentrix Shikangwa dakika ya 53 na 71, Mwanalima Jereko dakika ya 67 na Carazone Aquino dakika ya 87.

Saa 8:00 mchana Jumatatu Burundi itaanza kumenyana na Uganda katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kabla ya fainali kufuatia Saa 10:00 jioni.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE