Breaking News

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATATU NOVEMBER 25,2019

Mazungumzo ya kurefusha mkataba wa mshambuliaji Paris St-Germain Kylian Mbappe yanaendelea,huku rais wa klabu hiyo Leonardo akipatia umuhimu mkubwa hatma ya nyota huyo wa Ufaransa wa miaka 20. (L'Equipe - in French)

Newcastle United inamfuatilia Monaco beki Benoit Badiashile baada ya wasaka vipaji kumtazama kiungo huyo wa miaka 18-akicheza katika mechi ya klabu yake dhidi Bordeaux. (Newcastle Chronicle)

Kiungo wa kati wa Scotland na Aston Villa John McGinn, 25, atasalia Villa Park licha ya tetesi zinazomhusisha na uhaisho wa mwezi Januari. (Star)

Mchezaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, anayelengwa na Manchester United anasisistiza kuwa hana mpango wa kuondoka klabu hiyo Januari, japo winga huyo wa England anaonesha ari ya kutaka kuishi Ujerumani licha ya kujiona kama "kisababu" cha kutofanya vyema kwa klabu hiyo. (Athletic via Metro)

Chris Hughton na Rafael Benítez wako katika orodha ya kuchukua majukumu West Ham ikiwa mkufunzi wa klabu hiyo Manuel Pellegrini atafutwa kazi, baada ya kushindwa katika mechi saba. (Guardian)

Meneja mwingine wa Primia League ambaye anakabiliwa na wakati mgumu ni Unai Emery wa Arsenal huku meneja wa Juventus Max Allegri na msaidizi wa Manchester City Mikel Arteta wakitajwa kuwa katika orodha ya watu watakaochukua nafasi yake. (Mail)

Kocha wa Napoli, Carlo Ancelotti alihusishwa na tetesi ya kumrithi Mauricio Pochettino katika klabu ya Tottenham, lakini inadaiwa alikuwa "ghali mno" ndio sababu Spurs waliamua kumuakiri Jose Mourinho badala yake. (Mail)

Meneja wa Sheffield United, Chris Wilder pia anapigiwa upatu kuwa mkufunzi wa Hammers baada ya kuongoza klabu hiyo kufikia nafasi ya sita katika jedwali la msimamo wa ligi ya Premia. (Mirror)

West Ham wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Colombia Carlos Sanchez,33, mwezi Januari, mchezaji huyo akitarajiwa kuwa bila klabu msimu ujao. (Sun)

Tottenham inamfuatilia mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake, 24, huku beki huyo Mdachi akipigiwa upatu kuchukua nafasi ya Jan Vertonghen, ambaye kandarasi yake Spurs inakamilika msimu wa joto wa mwaka 2020. (Football Insider)

Leeds, Aston Villa na Crystal Palace zimeonesha ishara ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Rhian Brewster, 19, kwa mkopo ifikapo mwezi Januari. (Star)

Arsenal huenda ikamkosa beki wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti, 26, huku kiungo huyo wa Ufaransa ikipania kurejea katika klabu yake ya zamani ya Lyon ikiwa ataamua kuondoka Nou Camp. (L'Equipe - in French)

Beki wa kati na nyuma wa Wolves wa chini ya miaka 23, Owen Otasowie, 18, anatakiwa na mabingwa wa Ligue 1, Paris St-Germain na Schalke ya Bundesliga. (Sun)


Mchezaji wa Bournemouth Ryan Fraser amehusishwa na uhamisho wa kwenda Everton, Liverpool na Arsenal wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao, lakini winga huyo wamiaka 25 anasisitiza kuwa hajafikia uamuzi wa hatma yake ya siku zijazo. (mirror)
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE