TFF YATENGENEZA FURSA ZA KUKUZA SOKA KWA USHIRIKIANO NA UAE
Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia jana alifanya Mazungumzo na Rais wa Chama cha Soka cha Umoja wa Nchi za Falme ya Kiarabu Eng.Marwan Bin Ghalita kuhusiana na namna ya kukuza soka la vijana nchini.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Katibu Mkuu TFF Kidao Wilfred na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka UAE Mohamed Abdulla Hazzam Al Dhahari, mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama cha Soka UAE,pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali katika soka.
![](https://millardayo.com/wp-content/uploads/2019/11/WhatsApp-Image-2019-11-17-at-21.58.58-672x950.jpeg)