Breaking News

USAJILI WAONGEZEKA MARADUFU OSHA

Imeelezwa kuwa usajili wa maeneo ya kazi unaofanywa OSHA, umeongezeka zaidi ya mara sita (6) toka utekelezaji wa Blue Print uanze, hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda, wakati akifungua mafunzo  maalaumu ya usalama na Afya kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam.

Mwenda amesema, OSHA imetekeleza maagizo ya Mhe. Rais kwa kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma, ikiwemo kuondoa tozo na ada mbalimbali ambazo zilikuwa mzigo kwa wawekezaji nchini.
Kaimu Mtendaji huyo wa OSHA amesema tangu utekelezaji huo Blue Print uanze zaidi ya maeneo ya kazi elfu kumi na sita yamesajiliwa na OSHA  mpaka kufikia Juni 2019 ukilinganisha na maeneo 3354 yaliyosajiliwa mwaka 2015/2016.
Kwa upande wake washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu, na hivyo yatawasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku.
 OSHA imetekeleza maagizo ya Serikali ya kutaka kuondoa tozo zote ambazo zilikuwa kero hii ikiwa ni sambamba na ada mbalimbali ambazo zilikuwa mzigo ikiwemo ya usajili.
Miongoni mwa kodi ambazo OSHA wameziondoa ni pamoja na Ada ya usajili katika maeneo yote ya waajiri na sasa ni bure, Ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi, wamefuta faini zilizokuwa zikihusiana na vifaa vya kuzima moto, wameondoa Ada ya leseni, tozo ya ushauri wa kitaalamu ambayo walikuwa wakiitoza kila wanapokwenda kutoa ushauri wa kitaalamu na sasa haipo.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE