Breaking News

VIDEO: JPM AMWOKOA MPONDA KOKOTO ALIYEVUNJWA MKONO


RAIS John Magufuli ameutaka uongozi wa Wilaya ya Kahama kulishughulikia suala la mama mmoja mponda kokoto aliyesema alivunjwa mkono na mtu mmoja aitwaye Daudi lakini mtu huyo hajachukulia hatua yoyote.
Pamoja na hivyo, Magufuli alipitisha mchango wa fedha kumsaidia mama huyo wakati suala lake likishughulikiwa ili kumpunguzia matatizo aliyo nayo.


Rais  alifanya hivyo huku akiwataka viongozi hao wajifunze kushughulikia malalamiko ya wananchi badala ya kumsubiri yeye barabarani.


Kila kiongozi mtendaji aliamriwa kumchangia shilingi 50,000 na kufanikiwa kupata zaidi ya shilingi 500,000 papo hapo.

Pia Magufuli amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga kufuatilia sakata la mama huyo na kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa na sheria inafuata mkondo wake ili mama huyo apate haki yake.
FUATILIA TUKIO ZIMA HAPA
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE