WATATU WA SIMBA KUIKOSA RUVU SHOOTING LEO
LEO katika uwanja wa Uhuru Simba itakuwa na kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wao wa 10 wa Ligi Kuu Bara.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE
Patrick Aussems Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa yupo tayari kwa ushindani na anawaheshimu wapinzani wake ila atawakosa nyota wake watatu kutokana na sababu mbalimbali.
Nyota hao ni Erasto Nyoni na Sharaf Shiboub ambao wanasumbuliwa na majeruhi waliyoyapata kwenye timu zao za taifa huku Chama alichelewa kujiunga na timu akitokea kwenye timu ya taifa ya Zambia.