Breaking News

WAZIRI UMMY KUMFARIJI MTOTO ALIYEPOTEZA FAMILIA YAKE

Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameeleza kuguswa na tukio la kupoteza wazazi wawili, na ndugu zake watatu lililomkuta mwanafunzi Anna Zambi ambaye amemaliza kidato cha 4 hivi karibuni.

Ambapo Waziri Ummy ameahidi ataenda kumjulia hali mtoto huyo na kumpa salam za pole.

Ummy ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter mara baada ya mtoto huyo kupelekwa mahali ambapo wazazi wake na ndugu zake, baada ya kufariki Dunia walipokuwa wakielekea kwenye Mahafali yake ambapo walifariki Dunia wakiwa mkoani Tanga kutokana na mafuriko ya maji.

Waziri Ummy ameandika kuwa “hili jambo ni kubwa mno kwa mtoto Anna Zambi! inaumiza sana. ninamuombea kwa Mungu ampe nguvu na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

“Kama mzazi na Waziri mwenye dhamana ya Ustawi na Maendeleo ya Watoto nami nitamfikia Anna kwa ajili ya kumfariji na support nyingine.” ameongeza Waziri Ummy


Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo zake watatu, Lulu, Andrew na Grace walikufa katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa  wakisafiria kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Handeni mkoani Tanga.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE