Breaking News

YAFAHAMU MAMBO LUKUKI YALIYOMUONDOA AUSSEMS SIMBA


Katika mahojiano na kamati ya utendaji jana, YAFUATAYO YAMEMG'OA AUSSEMS SIMBA

1. Alipohojiwa ALIKWENDA WAPI BILA KUAGA ameshindwa KUJIBU pia AKAGOMA kutoa tiketi

2. AKAULIZWA Kwanini hakuaga kiofisi ameshindwa kutoa JIBU SAHIHI.

3. ALITAKIWA KUJIELEZA Kwanini haandiki RIPOTI za kazi kama inavyotakiwa, hakuwa na JIBU SAHIHI.

4. Suala la UBAGUZI kwa wachezaji pia kuwafokea na kudhalilisha bila kufuata weledi au kuwafukuza kwenye mazoezi, kwenye vyumba vya kubadili nguo na kwenye benchi mechi zikiendelea, HAKUWA NA MAELEZO SAHIHI.

5. Alikimbia kikao chake na CEO na Chairman HAKUWA NA MAELEZO

6. Alihojiwa tabia ya kuwatetea wachezaji WASIO NA NIDHAMU... hakuwa na JIBU sahihi.

7. Amekuwa akifanya juhudi kwa MAKUSUDI kuugombanisha uongozi na mashabiki na wanachama kupitia mitandao ya kijamii... ALIGOMA KUJIELEZA.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE