Breaking News

MJAMZITO ACHOMWA MSHALE TUMBONI

Mwanamke mmoja mjamzito, Sana Mohammad (35)mkazi wa London Uingereza ameuawa na mumewake kwa kuchomwa na mshale tumboni.
Imeelezwa kuwa mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Ramanodge (51) juzialihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumchoma na mshale tumboni mkewe aliyekuwa na mimba ya miezi tisa.
Licha ya mama huyo kufariki, kwa bahati nzuri mtoto aliyekuwa tumboni alitoka salama baada ya madaktari kuokoa maisha yake.
Imeelezwa kuwa wawili hao walikuwa wameachana na mwanamke huyo akaamua kuendelea na ukurasa mpya wa maisha na kubeba mimba ya mwanaume mwingine.
Awali wawili hao walifunga ndoa nchini kwao Mauritius, wakati huo Sana alikuwa na mika 16, baadaye walizaa watoto lakini ndoa yao haikuwa na amani kwani mwanaume alikuwa anamnyanyasa mkewe hadi akaamua kumkimbia na kuomba talaka.
Aliolewa na mwanaume mwingine ambaye waliishi kwa amani na upendo lakini mume huyo wa zamani aliamua kulipiza kisasi cha kuachwa kwa kuwaua wanandoa hao wapya licha ya kuishi vizuri na watoto wake.
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo aliuawa mbele ya wanae katika nyumba ya mume wake mpya, Imtiaz Mohammad.
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE