Breaking News

AZAM FC YAHITIMISHA TIMU 16 BORA (ASFC)

Klabu ya Azam FC imefunga mlango wa kuingia hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya jana kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Friends Rangers ya Daraja la Kwanza katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Azam FC ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo, sasa wataifuata Ihefu Jijini Mbeya kuwania tiketi ya Robo Fainali ya michuano hiyo.

Katika mchezo wa huo, mabao ya Azam FC yalifungwa na Iddi Kipagwile mawili katika dakika za 43 na 53 na Said Mourad aliyejifunga kwenye dakika ya 47 ambaye pia ndiye aliyefunga bao pekee la Friends Rangers dakika ya 85.

Azam FC imeungana na Yanga, Simba, Kitayosa, Namungo FC, Kagera Sugar, Stand United, Alliance FC, Ndanda SC, Ihefu FC, JKT Tanzania, Gwambina FC, Sahare All Stars, KMC, Panama na Mbeya City kuingia raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika hatua hiyo, mbali na Azam kuwa wageni wa Ihefu, Simba watakuwa watakuwa wageni wa Stand United, Yanga watakuwa wenyeji wa Gwambina, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa KMC, Ndanda wataikaribisha Kitayosa, Mbeya City wataikaribisha Namungo, JKT Tanzania wataikaribisha Alliance FC na Panama watakuwa wenyeji wa Sahare All Stars.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE