Breaking News

KUFUNGWA DIRISHA LA USAJILI: NANI KWENDA WAPI LEO?


Leo ni siku ya hekaheka kwa wahezaji, mawakala na makocha. Ijumaa ya leo Januari 31 ni mwisho wa dirisha dogo la usajili la majira ya baridi.

Kufikia saa sita ya usiku kwa saa za Ulaya timu nyingi zinatarajiwa kufanya makubaliano ya mwisho na kuuziana wachezaji.

Usajili mkubwa mpaka sasa kwa mwezi huu nchini Uingereza umefanywa na Manchester United jana Alhamisi kwa kumnyakua kiungo Bruno Fernandes kutoka klabu ya Sporting Lisbon.

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer aliahidi kuwa usajili huo ungekamilika kabla ya leo, na wametoa kitita cha pauni milioni 47. Hata hivyo dau hilo linaweza kuongezeka mpaka kufikia pauni milioni 67.

Je, wachezaji gani wanaoweza kusajiliwa leo?

Gareth Bale
Kumekuwa na tetesi zinazomhusisha winga wa kimataifa wa Wales Gareth Bale kuwa anataka kuihama klabu yake ya Real Madrid.

Tetesi hizo pia zinaihusisha klabu yake ya zamani Tottenham kuwa wanataka kumrejesha London.

Lakini ukweli ni upi? Na, je usajili huo unaweza kukamilika hii leo?
Japo Real ingependa kumuuza, lakini mpaka sasa hakuna klabu yoyote ambayo imeshapeleka ofa ya kumsajili mchezaji huyo mpaka sasa.

Hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa nyota huyo kubaki na miamba hiyo ya Uhispania.

Lakini yawezekana pia ikatumwa ofa ya dakika ya mwisho. Siku bado ndefu.

Olivier Giroud
Ni kama anaelekea nchini Italia ambapo vilabu vikongwe vya Inter Milan na Lazio vinaripotiwa kumtaka.

Klabu ya Chelsea inaonekana haina kikwazo kumuuza endapo watapata ofa.
Giroud pia amekuwa akihusishwa na kurudi Ligi ya Ufaransa.
Haitashtusha kusikia leo anapata klabu mpya.

Edinson Cavani
Yawezekana taarifa kumhusu Cavani ndizo ambazo zimezungumzwa zaidi mwezi huu.

Klabu kadhaa zimekuwa zikihusishwa kutaka kumnunua kuanzia Chelsea, Man United mpaka Atletico.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ulaya, Cavani amewaaga wachezaji wenzake wa PSG.

Lakini mpaka sasa klabu za PSG na Atletico hazijakubaliana bei ya usajili wa mchezaji huyo.

Antonee Robinson
Beki wa Wigan Athletic Antonee Robinson yuko katika harakati za kuhamia AC Milan kwa dau la £10m.

Mabingwa hao wa Serie A wamekuwa wakimnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa wiki kadhaa sasa na wanaaminika kuwasilisha ombi la kutaka kumsaini siku ya Alhamisi

Robinson alijiunga na Latics kutoka Everton mnamo mwezi Julai 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuonyesha mchezo mzuri alipokuwa katika uwanja wa DW.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE