Breaking News

MASTAA DUNIANI WAMLILIA BRYANT

JIJI la Los Angeles limekumbwa msiba kufuatia kifo cha Kobe Bryant katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili (jana).  Kifo cha mchezaji huyo wa mpira wa kikapu, aliyefariki na binti yake, Gianna,  kimewashtua watu wengi waliomfahamu, hususan watu maarufu sehemu mbalimbali duniani.
Miongoni mwa watu hao ni pamoja na waigizaji Christine Teigen na John Legend ambao ni mtu na mkewe.
Vilevile, bidada Khloe Kardashian, aliyekuwa na uhusiano na mchezaji wa karibu na Bryant aitwaye, Lamar Odom, alikumbwa na mshtuko mkubwa na kifo hicho ambapo yeye na dada yake,  Kim Kardashian, mama yao, Kris Jenner, walielezea masikitiko yao kwa kifo cha nyota  huyo na binti yake.
Staa wa muziki, Kanye West, ambaye pia ni mme wa Kim Kardashian, alisambaza kwenye mitandao picha yake na Kobe Bryant waliyopiga wakiwa pamoja siku za nyuma.
Lebron James akimwaga machozi.
Mastaa wengine walioomboleza kifo hicho ni waimbaji  Bruno Mars, Pink, Lizzo, na  Ciara.
Mwimbaji Mariah Carey, na mtunzi wa vitabu Stephen King ni baadhi tu ya watu maarufu duniani walioshiriki katika kuomboleza kifo cha Bryand ambaye alikuwa nyota wa timu ya Lakers kwa miaka 20.

Mchezaji Neymar alifunga mabao mawili kwenye mchezo kati ya #PSG dhidi ya #Lille. Neymar ameonekana kuyaelekeza magoli haya kwa #KobeBryant aliyefariki muda mfupi uliopita kwa ajali ya helikopta.

Neymar alionekana akionyesha Ishara ya namba 24 kwa kutumia vidole vyake kabla ya kumalizia kwa ishara ya kumwombea #KobeBryant.

Baadhi ya ujumbe uliotumwa na mastaa na watu mashuhuri kuhusiana na kifo cha mwanamichezo huyo zinafuatia chini:
                
UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE