Breaking News

MSUVA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA EL JADIDA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Saimon Msuva ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019 wa klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Msuva ameshinda tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika usiku wa jana.


“Nimechukua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019 ndani ya klabu yangu ya Difaa El Jadida si ligi. (tuzo zinazoandaliwa na klabu) mimi ndiye nimeshinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu,” amesema Msuva.

UPDATE NIJUZE HABARI APP, CLICK HERE